Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morocco yatishia kususia mashindano ya Afrika

Morocco To Quarter Final Morocco yatishia kususia mashindano ya Afrika

Thu, 29 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya taifa ya Morocco imetishia kususia kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani kutokana na mvutano na Algeria.

Baada ya mafanikio makubwa iliyoyapata kwenye michuano ya Kombe la Dunia, timu ya taifa ya Morocco huenda ikasusia kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani - CHAN itakayofanyika mwezi ujao kutokana na mvutano wa kidiplomasia na mwenyeji wa michuano, Algeria.

Shirikisho la Soka la Morocco limesema limeandika barua kwa Umoja wa Afrika likishinikiza timu yake kusafiri moja kwa moja kwa kutumia ndege binafsi ya shirika la Royal Air Maroc kutoka mji mkuu Rabat hadi hadi jiji la Constantine nchini Algeria ambako kutafanyika michuano hiyo.

Ndege za jeshi na za kibiashara za nchini Morocco zimezuiwa kupita katika anga ya Algeria tangu majirani hao wawili walipovunja mahusiano ya kidiplomasia mwaka jana, kutokana na masuala kadhaa ambayo ni pamoja na eneo linalozozaniwa la Sahara Magharibi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live