Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morocco yakata rufaa mechi yake dhidi ya Ufaransa

Operanews1671162002772 Morocco yakata rufaa mechi yake dhidi ya Ufaransa

Fri, 16 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Soka la Morocco (FRMF) limetangaza Alhamisi, Desemba 15, kwamba limewasilisha malalamiko yake kwa 'chombo chenye uwezo' (bila kutaja jina) kupinga usimamizi wa mechi ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Dunia 2022, ambapo Simba wa Atlas walifungwa na Ufaransa 2-0 siku ya Jumatano.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, FRMF inarejea kwenye maamuzi mawili ya ussimamizi wa mechi "baada ya kuinyima Morocco penalti mbili zisizopingika kwa maoni ya wataalamu kadhaa".

Shirikisho la soka la Morocco linazungumzia kitendo kilichotokea katika dakika ya 27 wakati Sofiane Boufal na Théo Hernandez walipokutana katika eneo hilo, na ambapo mwamuzi kutoka Mexico, César Arturo Ramos, alitoa onyo kwa Morocco.

Shirikisho hilo pia limekosoa kutopigwa kwa penalti ambayo mwamuzi alikubali mwenyewe, kabla ya mapumziko, wakati Youssef En-Nesyri alijikuta amedondoshwa baada ya kugongana na Aurélien Tchouaméni. FRMF inashangaa kwamba mwamuzi kupitia video "haikujibu hali hizi". Rufaa yake kwa hakika haina nafasi ya kushinda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live