Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morocco walikuwa bora, huo ndio ukweli - Samatta

Video Archive
Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta ametoa maoni yake kuhusu mchezo wa Taifa Stars dhidi ya Morocco uliomalizika kwa Stars kupoteza 3-0 katika uwanja wa Laurent Pokou nchini Ivory Coasta yanakochezwa mashindano ya AFCON 2023.

Akizungumzia hilo baada ya mchezo huo kumalizika na Stars kuchabangwa bao 3-0 dhidi ya Morocco, Samatta ameweka wazi kuwa Morocco walikuwa bora kuliko Stars na ukweli lazima usemwe ili watu wajue.

"Morocco walikuwa bora hilo lazima tukubali, tulijaribu kucheza kwa discipline na kufuata maelekezo ya walimu lakini Morocco walikuwa bora. Walipata bao la kwanza kupitia mpira wa adhabu.

"Baada ya kutanguliwa ilikuwa ngumu kwa Timu ya Taifa ya Tanzania kwa sababu unapocheza na mpinzani kama Morocco na akakutangulia, wana wachezaji ambao wanaweza kumiliki mpira kwa muda mrefu inakuwa ngumu kutengeneza nafasi na kupata mabao.

"Kwa hiyo inabidi tukubali kuwa walikuwa bora, mechi imeshaisha hatuwezi kubadilisha matokeo, inabidi tu-focus katika mechi ya dhambia ambayo inakuja mbele," amesema Samatta.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live