Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morocco wakutana na kichapo mbele ya Croatia

Croatia 3rd Timu ya Croatia wakishangilia ushindi baada ya kufanikiwa kukamata nafasi ya tatu

Sat, 17 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wawakilishi wa Bara la Afrika kunako michuano ya Kombe la Dunia, Timu ya Taifa ya Morocco imehitimisha safari yake hii leo kwa kichapo cha magoli 2-1 kutoka kwa Croatia.

Morocco walikuwa na kibarua mbele ya Croatia, mechi ya kusaka mshindi wa tatu wamekubali kipigo hicho na kujikuta wakimaliza nafasi ya nne hivyo kushindwa kuvaa hata medali ya mshindi wa tatu.

Magoli ya Croatia yamefungwa na mlinzi J. Gvardio dakika ya 7, lakini dakika ya 9, Morocco wakasawazisha kupitia kwa A. Dari.

Bao la pili la Croatia limepachikwa na M. Orsic dakika ya 42 na mpaka mchezo huo unakwenda mapumziko, Croatia walikuwa mbele kwa magoli 2-1.

Mpaka dakika 90 zinakamilika mchezo huo uliwashuhudia Croatia wakiibuka wababe mbele ya Morocco ambao kwa mara ya kwanza wameweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutoka Afrika kufika hatua ya nusu Fainali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live