Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morocco waisimamisha Bendera ya Afrika Qatar, waitoa Hispania

Morocco To Quarter Final Morocco imefuzu hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza

Tue, 6 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Taifa ya Morocco imefanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Qatar.

Morocco inafuzu hatua hiyo bada ya kufanikiwa kuiondoa Timu ya Hispania kwa mikwaju ya penati 3-0 baada ya kumalizika dakika 90 kwa sare ya bila kufungana na kuongezwa dakika 30 huku matokeo yakibaki vile vile 0-0.

Hispani walitawala sehemu kubwa ya mchezo huku Morocco wakijilinda kwa nidhamu ya hali ya juu kwa dakika zote 120 za mchezo.

Kama si uhodari wa mlinda lango wa Morocco Bono, Hispani wangepata bao dakika za mwishoni kabisa lakini alifanikiwa kuzuia mashambulizi mawili ya hatari.

Morocco wanakua timu pekee ya Afrika kufika hatua ya Robo Fainali baada ya Ghana, Cameroon na Tunisia kuondolewa hatua ya Mkaundi huku Senegal wakiondolewa hatua ya 16 bora.

Hispania waliokosa penati ni P. Sarabia, C. Soler na Nahodha Sergio Busquets huku Morocco wakipata penati 3 zilizofungwa na Ziyech, Hakimi, A. Sabiri huku mchezaji B. Benoun akikosa kwa upande wa Morocco.

Katika hatua ya Robo Fainali Morocco watakutana na mshindi kati ya Ureno dhidi ya Switzerland wanaoshuka dimbani majira ya saa nne usiku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live