Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morocco atoa ahadi Geita Gold

Hemed Morocco Kocha Morocco atoa ahadi Geita Gold

Tue, 24 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Licha ya kikosi chake kutokuwa na matokeo ya kuridhisha kwenye Ligi Kuu Bara, Kocha Mkuu wa Geita Gold, Hemed Sulemani ‘Morocco’ amesema anaridhishwa na jinsi kikosi chake kinavyoimarika huku akiwa na uhakika mashabiki wataanza kufurahi muda siyo mrefu.

Timu hiyo haijapata ushindi katika mechi tano mfululizo za mashindano hayo, ikipoteza tatu na sare mbili, ambapo wikendi iliyopita ililazimishwa sare ya 2-2 na Dodoma Jiji katika Uwanja wa Nyankumbu, mkoani Geita.

Matajiri hao wa dhahabu wanashika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi tano katika mechi sita walizocheza, wakishinda moja, sare mbili na kupoteza tatu, huku wakifunga mabao manne na kuruhusu nane.

Akizungumza baada ya sare ya 2-2 na Dodoma Jiji katika Uwanja wa Nyankumbu, Morocco alisema timu yake ni mpya na bado anaendelea kuijenga na tayari ameanza kuona mabadiliko katika kikosi chake hivyo anaamini ushindi utaanza kupatikana.

“Ni kweli bado kuna presha wachezaji wanapigana kupata matokeo lakini ni kitu cha kawaida kwenye klabu wakati ambao mnakosa matokeo, lakini tunapiga hatua na kuimarika kulinganisha na mechi mbili zilizopita,” alisema Morocco na kuongeza;

“Jambo la muhimu tunarudi kwenye kiwanja cha mazoezi na kujaribu kufanyia kazi kile ambacho kimeonekana leo, tuna timu mpya najaribu kuijenga ni suala la muda kila kitu kitakuwa sawa,”

Chanzo: Mwanaspoti