Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morocco alivyomuibua Bacca, Wananchi wanampigia salute Jangwani

Bacca Yanga Morocco alivyomuibua Bacca, Wananchi wanampigia salute Jangwani

Fri, 3 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati kocha Hemed Suleiman Morocco anatangaza kikosi cha Zanzibar Heroes mwaka 2017 ambacho kinaenda kushiriki mashindano ya CECAFA Senior Challenge pale nchini kenya kwenye list ya wachezaji lilikuwemo jina la Ibrahim Bacca.

Hii ilipelekea wadau wengi wa soka Visiwa zanzibar kujiuliza kocha Morocco anamuiita huyu Bacca kwenda kufanya nini wakati kipindi hicho Zanzibar Heroes ilikuwa na mabeki visiki kama Abdallah Shaibu Ninja, Issa Haidar Dau, Abdallah Kheir, na Mohamed Othman Mmanga pia kipindi hicho Ibrahim Bacca alikuwa na umri mdogo sana.

Kocha Hemed Suleiman Morocco alisema anamchukua huyu nimeona ana kipaji na anaenda kupata uzoefu na kujifunza zaidi kupitia wenziwe.

Ni kweli baada ya Zanzibar kufika kenya kwenye mashindano hayo Ibrahim Bacca hakuwa mchezaji wa kupata nafasi kwa maana nafasi ya beki za kati yaani ni 4 na 5 ilisimamiwa kikamilifu na Issa Haidar Dau na Abdallah Kheri Sebo.

Kuna baadhi ya mechi kama ile dhidi ya Libya ambapo Zanzibar ilipasuka kwa 1-0 beki aliyepata nafasi alikuwa ni Abdallah Shaibu Ninja, japo kuna baadhi ya game Bacca alipata nafasi kwa dakika chache sana.

Pale visiwani Zanzibar kuna Mchambuzi wa soka anaitwa Hussein Ahmada ni moja ya wachambuzi wazuri sana na katika makala zake aliwahi andika na kupost Ibrahim Bacca kipindi yupo Klabu ya Malindi kuwa ni talent kubwa sana.

Miongoni mwa vijana watakao kuja kuwa mabeki wakubwa sana nchi na hii leo ni kweli Ibrahim Hamad Abdullah ni moja ya mabeki bora na mahiri hapa Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live