Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morocco alia na ubora wa wachezaji Namungo

Nkana 6 Pic Data Morocco alia na ubora wa wachezaji Namungo

Mon, 5 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

BAADA ya jana Jumapili kupokea kipigo cha tatu mfululizo katika Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi kutoka kwa Nkana ya Zambia, Kocha Mkuu wa Namungo Hemed Morocco amesema kinachomponza ni ubora wa wachezaji wake.

Namungo ikiwa nyumbani jana kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa iliruhusu kufungwa bao 1-0 bila na Nkana walioonekana kumudu mchezo kwa muda mwingi, bao hilo likiwekwa nyavuni na Diamond Chikwekwe dakika ya 69.

Baada ya mchezo huo Mwanaspoti ilizungumza na kocha mkuu wa Namungo, Hemed Morocco ambaye aliweka wazi kuwa tatizo kubwa linalofanya kupoteza michezo ya kimataifa ni ubora na uzoefu wa wachezaji wake kuwa mdogo.

“Tumepoteza mchezo wa tatu mfululizo hatua hii ya makundi, hatuna cha kulaumu sana kutokana na maandalizi yetu na kinachotuponza zaidi ni ubora wa wachezaji wetu kutoendana na mashindano tuliyopo.

Tuna wachezaji wazuri lakini wengi wao hawana uzoefu wa mashindano makubwa kama haya hivyo huwa inatokea shida pale wanapokutana na timu zenye majina makubwa na wachezaji wakubwa lakini pamoja na hayo tunaendelea kuwa imara kwaajili ya siku zijazo,” amesema Morocco.

Ikiwa kundi D pamoja na timu za Raja Casablanca ya Morocco, Pyramids ya Misri na Nkana ya Zambia haijapata ushindi wote wala sare katika michezo yote mitatu ya kwanza kwani wamefungwa 1-0 na Raja ugenini, wakapoteza nyumbani kwa kupigwa 2-0 na Pyramids na jana wamelala 1-0 kwa Nkana.

Related Nkana yafufukia Dar, Namungo chali tena kwa Mkapa Nkana yapasha nje ya uwanja wakiivutia kasi Namungo Wachezaji Nkana waimba na kucheza nje ya uwanja Nkana waingia uwanjani baada ya dakika 37Mchezo unaofuata katika michuano hiyo, Namungo atacheza na Nkana Aprili 11 ugenini nchini Zambia.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz