Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morocco, Hispania, Ureno kuandaa Kombe la Dunia 2030

World Cup 2030 Morocco, Hispania, Ureno kuandaa Kombe la Dunia 2030

Wed, 15 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Morocco imetangaza maombi ya pamoja na Uhispania na Ureno ya kuandaa Kombe la Dunia la FIFA 2030 ikichukua nafasi ya Ukraine ambayo awali ilikuwa kwenye mpango huo wa pamoja.

Mpango wa kuandaa Kombe la Dunia wa kuvuka mabara kati ya Uhispania, Ureno na Morocco, unatajwa kuwa na manufaa kadhaa, ikizingatiwa tayari kuna miundombinu thabiti katika nchi hizo tatu. Wakati huo huo, ukaribu wa Nchi hizo kijiografia utarahisisha usafiri kuliko kwa zabuni zingine.

Fainali za Kombe la Dunia 2030 zitashirikisha timu 48 na hii inaongeza wigo wa kuwa na viwanja vingi, kama ilivyo kwa Kombe la Dunia la 2026 litakalofanyika Amerika, Canada na Mexico.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live