Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moro, Mkundi Youth mambo magumu U20

Moro Pic 3333 Moro, Mkundi Youth mambo magumu U20

Sat, 7 May 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Wakati Ligi ya vijana chini ya umri wa miaka 20 wilaya ya Morogoro 2022 ikiendelea na kupambamoto, mambo sio mazuri kwa timu ya Moro Youth na Mkundi Youth ambazo hazijaonja ladha ya ushindi tangu kuanza kwa michuano hiyo.

Moro Youth iliyo chini ya Taasisi ya Kukuza na Kuendeleza Vipaji vya Soka Morogoro imejikuta ikishindwa kutamba mbele ya wapinzani wao na kupokea vipigo katika michezo yake licha ya timu hiyo kuwa na vijana wengi wenye vipaji vingi vya soka.

Katika mchezo wa kwanza Moro Youth imejikuta ikiadhibiwa kwa kipigo cha bao 2-1 dhidi ya Mega Sports Club huku mchezo wa pili ikikubali kipigo kingine cha bao 2-0 mbele ya Fountain Gate Academy na mchezo wake wa tatu ikipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya ya Kilombero Soccer Net katika michezo hiyo inayofanyika uwanja wa Sabasaba Manispaa ya Morogoro.

Kutokana na matokeo hayo, Moro Youth inajiweka katika hatari ya kusonga mbele kwa kuwa na matumaini madogo ikiwa imebakisha michezo tatu ili kuona kama inaweza kupata matokeo na kufufua matumaini ya kusonga hatua inayofuata.

Akizungumza mkoani hapa, Katibu wa chama cha soka wilaya ya Morogoro (MDFA), Geofrey Mwatesa alisema Moro Youth na Mkundi Youth ni miongoni mwa timu ambazo hazijaonja radha ya ushindi tangu mashindano hayo yaanze kutimua vumbi wiki moja iliyopita kwa kushindwa kuonyesha cheche.

Mwatesa alisema Moro Youth licha ya kupoteza michezo mitatu bado wana wachezaji wanaoonyesha uwezo nzuri katika michezo hiyo kutokana na vipaji vya soka na huenda bahati haiko katika upande wao dhidi ya wapinzani wao.

“Mashindano haya ni mazuri, timu zote 21 zina vijana wanaoonyesha uwezo mkubwa katika soka na hii ni kwa sababu kuna vipaji vingi vya soka na hali ya kutopata matokeo imeikuta pia Mkundi Youth ambayo nayo imepoteza michezo yake yote miwili ya michezo hiyo nina imani watakuja kuimarika katika michezo iliyobakia kwao.”alisema Mwatesa.

Wakati Moro Youth, Mkundi Youth ikibolonga katika michezo yao, unaambiwa mshambuliaji wa timu ya Moro Kids, Baraka Lutz anafurahia kufunga Hat Trick ya kwanza katika michuano hiyo baada ya timu yake kupata ushindi mnono wa bao -0 mbele ya Save Talents.

Lutz alisema mashindano hayo anayatumia kujifunza zaidi mbinu za kufunga mabao kwa kufuata maelekezo ya benchi la ufundi la timu yao ili wawe wanaibuka na ushindi kwa kila mchezo dhidi ya wapinzani wao na kutimiza ndoto zao za kufika fainali na kutwaa kombe.

“Mchezo wetu wa kwanza tulipoteza na mchezo wa pili tumeibuka na ushindi wa bao 5-0 na nimefurahi kufunga Hat Trick ya kwanza katika haya mashindano nayatumia kunifunza zaidi namna ya kufunga kwani lengo la timu ni kutwaa ubingwa na nimejiwekea lengo la kuwa mfungaji bora hivyo nahitaji kufunga zaidi.”alisema Lutz.

Lutz alisema michuano hiyo binafsi itamuirisha zaidi pamoja na wachezaji wenzake kwa kupanua zaidi akili katika uchezaji soka kwa kuzingatia wanakutana na vijana wenzao ambao wana vipaji kama wao kutoka academy mbalimbali.

 

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz