Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morisson Huru Kuichezea Simba, Yanga Hawajakata Tamaa

Morrison.jpeg Bernard Morisson

Tue, 12 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa timu ya Simba, Bernard Morisson amemaliza adhabu yake ya kutokucheza michezo 3 ya mashindano Tanzania bara, baada ya kutenda kosa la kinidhamu katika mchezo wa Fainal ya FA, Julai 25, 2021.

Bernard Morisson ambae kwa kawaida huwa haishiwi na vituko, alikutana na adhabu kubwa ambayo iliambatana na faini ya pesa pamoja na kufungiwa kucheza michezo mitatu ya Mashindano Tanzania bara, kutokana na kitendo chake cha kuvua nguo uwanjani mara tu, baada ya mchezo kumalizika wa Fainal ya FA uliozikutanisha Simba na Yanga.

Ifahamike kuwa Simba katika mchezo huo wa Fainal iliibuka na Ubingwa huo wa Kombe la Shirikisho Tanzania bara, ndipo furaha ikazidi kina na Morisson akajikuta anavua bukta yake na kuivaa kichwani, Jambo ambalo lilizua utata mkubwa ndio TFF ikaamua kumfungia nyota huyo na kumlima faini, ili iwe fundisho kwa wachezaji wengine pia.

Kwa maana hiyo Winga huyo hatari wa Klabu ya Simba atarejea katika michezo inayofuata ya Simba ambapo, Simba kwa sasa imerejea Jijini Dar es Salaam, baada ya kumaliza michezo yake ya Mkoani miwili na kujikusanyia alama 4 kibindoni. Urejeo wa Bernard Morisson katika timu ya Simba, utaongeza Jambo kubwa katika kikosi hicho kutokana na ubora wa nyota huyo awapo uwanjani.

Ifahamike kuwa Simba tokea, imeanza kucheza katika msimu huu wa 2021/2022 ilikuwa haijapata ushindi wowote na hatimae Octoba 01, 2021 wamejipatia ushindi wao wa kwanza dhidi ya Dodoma Jiji, mchezo uliochezwa Jijini Dodoma na Simba ikaubuka na Ushindi wa Goli 1 kwa bila, goli ambalo lilifungwa na Medie Kagere.

Kwa upande wa Kesi ya Mchezaji Bernard Morisson na timu yake ya Yanga ambayo inasubiriwa na mashabiki wengi kwa hamu kutaka kusikia nini kitaamuliwa Octoba 15, 2021 kule CAS kama ambavyo Yanga wenyewe walitangaza, mwezi uliopita yaani Septemba.

Ifahamike kuwa kesi ya mchezaji Bernard Morisson na Yanga kwa Sasa imetimiza mwaka sasa, huku mashabiki wa Yanga walio wengi wakiwa na imani kwamba watashinda katika kesi hiyo. Lakini ifahamike kuwa kwa sasa kinachosubiriwa ni CAS kutoa hukumu ya kesi hiyo ambayo Yanga ndio walalamika kwa Mchezaji huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live