Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morata hatihati kuikosa fainali

Alvaro Moratta Miss Morata hatihati kuikosa fainali

Thu, 11 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Ikiwa ni siku kadhaa tangu mshambuliaji wa Atletico Madrid, Alvaro Morata kusema anafikiria kuachana na timu ya taifa ya Hispania, huenda akakosekana katika mchezo wa fainali baada ya kuumia.

Morata aliumia bahati mbaya kutokana na mlinzi wa uwanja huo kuteleza na kumvaa miguuni baada ya mchezo wao wa nuysu fainali dhidi ya Ufaransa.

Tukio hilo lilitokea baada ya shabiki mmoja kuvamia uwanjani akijaribu kujiunga na sherehe za Hispania baada ya ushindi wao wa mabao 2-1 na mlinzi huyo aliamua kujaribu kumzuia shabiki huyo lakini aliteleza na kumkwaa mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea miguuni.

Baada ya tukio hilo, Morata alionekana kuwa na maumivu makali huku akizungukazunguka akiugulia wakati wachezaji wenzake wakishangilia.

Tukio hilo limezua wasiwasi ikiwa staa huyo atacheza fainali wikiendi hii kwani haijajulikana amepata majeraha kiasi gani.

Kocha wa Hispania, Luis de la Fuente alipoulizwa juu ya tukio hilo alisema: “Tutasubiri hadi kesho kuona inakuwaje, kwa sasa hatuna majibu, ni kweli mguu unamuuma lakini nina matumaini atakuwa sawa.

Morata aliiongoza timu yake katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ufaransa, uliomfanya Lamine Yamal kuweka historia.

Bao lake la maajabu la umbali wa yadi 25 liliifanya Hispania kusawazisha baada ya Ufaransa kuongoza kwa bao la Randal Kolo Muani.

Pia ilimfanya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi mdogo kufunga bao katika historia ya Euro, akiwa na umri wa miaka 16 na siku 362.

Mapema wiki hii Morata alitishia kuacha kucheza soka la kimataifa, kutokana na kukosolewa na kusemwa vibaya na mashabiki wa taifa hilo.

“Inaweza kuwa michuano yangu ya mwisho na Hispania, sitaki kuzungumza sana lakini kuna uwezekano huo, nikiwa Hispania imekuwa ngumu kwangu kuw ana furaha,” alisema Morata.

Chanzo: Mwanaspoti