Mshambuliaji wa Atletico Madrid na Timu ya Taifa ya Hispania, Alvaro Morata, amefunguka kuwa kiungo wa Real Madrid na timu ya Taifa ya Croatia, Luka Modric hahihitaji taji kuonesha chochote kwani ukweli unabaki kuwa yeye ni mchezaji bora.
Hii ni baada ya kiungo huyo wa Croatia kukosa taji la UEFA Nations League hivi karibuni wakati wakicheza fainali dhidi ya Hispania.
Modric ndani ya Madrid, amecheza kwa mafanikio makubwa na kushinda kila taji waliloshindania, lakini kwa timu ya taifa amekuwa hana bahati, akifika fainali Kombe la Dunia 2018 na 2022 akiishia nusu fainali, huku UEFA Nations League 2023 akipoteza fainali.
Morata alisema: “Nafikiri kuwa Luka Modric hahitaji tuzo wala taji lolote ili kuonesha yeye ni bora, kwani dunia ya soka inatambua ubora wa kiungo huyo, amekuwa akipambana na hata akistafuu leo hana deni, anastahili heshima.”