Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mopa agoma kurusha taulo Geita Gold, Kocha afafanua

Pic Kyaruzi Mopa agoma kurusha taulo Geita Gold, Kocha afafanua

Wed, 22 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Licha ya kutopata namba katika kikosi cha Geita Gold, beki mpya wa timu hiyo, Erick Kyaruzi 'Mopa' amesema hawezi kukata tamaa mapema kwani ana matumaini makubwa ya kupewa nafasi na benchi la ufundi la timu hiyo kutokana na uzoefu mkubwa alionao na bidii mazoezini.

Kyaruzi alijiunga na Geita Gold dirisha dogo akiwa mchezaji huru kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya kumalizana na Kagera Sugar mwishoni mwa msimu uliopita na kukosa timu ya kuichezea dirisha kubwa.

Tangu ametua hapo Januari, mwaka huu beki huyo wa zamani wa Kagera Sugar, hajacheza mchezo wowote wa kimashindano huku akiishia benchi ukiwamo mchezo uliopita walioshinda mabao 3-2 dhidi ya Ruvu Shooting huku akiwa sehemu ya wachezaji wa akiba.

Akizungumza Kyaruzi alisema hawezi kukata tamaa ya kukosa namba kwani anaamini muda utafika atacheza huku akiitamani pacha yake na Kelvin Yondani kutokana na uzoefu wao kwani wanaweza kutengeneza muunganiko mzuri.

"Nipo napambana sana ni muda tu wakupata nafasi najua nitakaa poa kwa sasa bado nakaa benchi lakini namshukuru Mungu naamini nitapata nafasi ya kucheza na kuisaidia timu yangu.

"Ni kweli timu yetu ina wachezaji wazuri na wazoefu kama Kelvin Yondani katika eneo la ulinzi lakini sina wasiwasi wa kupata namba kwa sababu ni kupambana tu na mpira ni mchezo wa nafasi, mimi ni mkongwe pia naamini nafasi ikipatikana tu ni kuitendea haki cha muhimu timu inapata matokeo mazuri," alisema kitasa hiyo.

Beki huyo wa zamani wa Mbeya City, aliwapongeza mashabiki wa timu walivyowapokea kwa mikono miwili wachezaji wao na kuwapa sapoti kila mchezo wanapocheza nyumbani (Nyankumbu), huku akiwaomba waendelee kuwaunga mkono kwa nguvu kubwa katika michezo iliyobaki ili wachezaji wazidi kujituma na kupata matokeo mazuri.

Kocha Msaidizi wa Geita Gold, Mathias Wandiba alisema benchi lao limejijengea utamaduni wa kumuamini kila mchezaji ambaye amesajiliwa na timu hiyo ambapo kila mmoja atapata nafasi ya kucheza kutokana na kile anachokifanya mazoezini, aina ya mchezo wanaokabiliana nao na kutoa nafasi ya kila mmoja kuonyesha uwezo wake.

Chanzo: Mwanaspoti