Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moloko ajipa majukumu mazito Yanga

YANGA MAYELE MOLOKO FEI TOTO Moloko apanga kuwarahisishia kazi washambuliaji

Tue, 9 Nov 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Winga ya Yanga, Jesus Ducapel Moloko, amesema atahakikisha anaongeza juhudi katika kutengeneza nafasi kwa washambuliaji wao wakiongozwa na Fiston Mayele ili yapatikane mabao mengi.

Moloko amejiunga na Yanga msimu huu akitokea AS Vita ya DR Congo ambapo mpaka sasa ndani ya Ligi Kuu Bara amefanikiwa kufungia mabao mawili katika mechi tano, huku akiwa hana asisti.

Akizungumza na Spoti Xtra, Moloko aliweka wazi matanio yake ya kutengeneza nafasi nyingi za kufunga kwenda katika idara ya ushambuliaji huku akisema atahakikisha anaongeza juhudi kufanikisha hilo.

“Katika nafasi ambayo nacheza vitu vya msingi kwangu ni kutengeneza mabao pamoja na kufunga, tayari nimefanikiwa kutimiza moja lakini lingine bado sijafanikiwa.

“Natakiwa kutengeneza nafasi nyingi zaidi kwenda kwa washambuliaji ili waweze kufunga mabao ya kutosha, natamani kuona hilo nilikifanya.

“Bado kuna michezo mingi, nitapambana kuhakikisha safu ya ushambuliaji nawapikia mabao ya kutosha, nafahamu haitakuwa kazi nyepesi, lakini nitapambana kuhakikisha nafanikiwa,” amesema winga huyo raia wa DR Congo.

Chanzo: globalpublishers.co.tz