Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moloko aibukia Mtibwa ya Libya

Ducapel Molokoo Jesus Moloko

Tue, 30 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika Ligi Kuu Bara ni timu mbili ambazo zimeshinda mechi chache zaidi hadi sasa ikiwa ni Mashujaa FC na Mtibwa Sugar zilizoshinda mara mbili kati ya tisa.

Nchini Libya kwenye msimamo ni timu tatu zimenasa mkiani. Moja ni Al Sadaga iliyoshinda mechi moja kati ya timu ilizocheza. Timu hiyo imemsajili winga wa zamani wa Yanga, Jesus Moloko aliyesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia huku akiweka wazi kuwa anakwenda kupambana.

Moloko ametimkia nchini Libya baada ya kumalizana na Yanga aliyoitumikia kwa misimu miwili akitwaa mataji mawili ya ligi na Ngao ya Jamii moja.

Akizungumza na Mwanaspoti kwa simu akiwa nchini DR Congo, alisema amemalizana na timu hiyo na yupo tayari kwa ajili ya ushindani.

“Baada ya Tanzania sasa ni wakati wa Libya. Ni nchi ngeni kwangu lakini soka limenipeleka huko kwa lengo la kutafuta changamoto nyingine. Naamini katika kupambana hivyo kila kitu kinawezekana,” alisema.

“Sijawahi kucheza huko lakini hilo haliwezi kunipa uhuru wa kuacha kukitumikia kipaji nilicho nacho. Malengo ni kuisaidia timu hiyo kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu kuhakikisha tunafikia malengo.”

Moloko alisema ni wakati sahihi kwake kupata timu kipindi hiki akiwa katika hali ya ushindani baada ya kutoka Yanga huku akikiri kuwa anaamini kila kitu kitakwenda kama alivyopanga akiwa nchini humo.

Moloko atakuwa na kazi ya kuipambania timu hiyo kutoshuka daraja kwani ipo nafasi ya nane kwenye msimamo wa timu 10 ikiwa imeshinda mchezo mmoja, sare tatu na kufungwa tano kati ya tisa ilizocheza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live