Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moloko, Mzize walivyoinusuru Yanga CCM Mkwakwani

Moloko, Mzize Walivyoinusuru Yanga CCM Mkwakwani.jpeg Moloko, Mzize walivyoinusuru Yanga CCM Mkwakwani

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jesus Moloko na Clement Mzize ndio ambao walibadilisha matokeo jana ya Yanga SC baada ya Wananchi hao kubanywa vilivyo mpaka zaidi ya dakika ya 70 bila kupata matokeo.

Baada ya kuona hivyo, mwalimu Miguel Ángel Gamondi akaona jahazi linazama ndipo alipolazimika kumuingiza Moloko na Mzize ambao ndio walikwenda kuifungua safu ya ulinzi ya Coastal Union.

Yanga wakaanza kushambulia kwa kupitia pembeni na hatimaye dakika ya 71, Moloko akamwaga maji, Mzize akashusha heda nzuri ambayo ilizama nyavuni.

Mpaka mwisho wa mchezo, Yanga 1-0 Coastal. Yanga wamezidi kujikita kileleni wakiwa na alama 24 baada ya kucheza mechi 9 za Ligi Kuu ya NBC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live