Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Molinga amtaka Mayele kutuliza akili

Mayele, Lomalisa Moloko David Molinga

Wed, 21 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, David Molinga amesema ni vyema wachezaji wote wanaocheza soka nchini Tanzania wakafanya maamuzi sahihi katika kipindi hiki cha usajili.

Molinga amesema ni kweli wachezaji wameonyesha kiwango kizuri, na uzuri mitandao na majukwaa mbalimbali Tanzania ina nguvu ndio maana wanaonekana kwa hao wengine wanaowahitaji sasa.

Nyota huyo anayekipiga Saudi Arabia amemgusia mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele kuwa ni mchezaji msikivu, na anaziona taarifa zinazomhusisha kwamba anatakiwa na klabu nyingine

Molinga amemtaka Mayele kutuliza akili, na aone sehemu sahihi itakayomfanya acheze kwa furaha, amesisitiza kuwa wakati mwingine unaweza kuondoka sehemu ambayo unafunga mabao na kuonekana, halafu unapokwenda mambo yakawa tofauti.

Suala hilo amesema sio kwa Mayele peke yake bali ni ushauri kwa wachezaji wote wa Congo wanaocheza Tanzania.

Molinga amesema ipo tofauti kubwa kati ya nchi alizowahi kucheza na hapa Tanzania ambapo anasema watu wake wanapenda sana mpira na wakikukubali unafurahia maisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: