Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Molinga aichambua Yanga ya Gamondi

Aziz Chama Pacome Yanga Molinga aichambua Yanga ya Gamondi

Fri, 2 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji Sohar Fc ya nchini Oman, David Molinga amesema kuwa kwa sasa mchezaji kupata nafasi ndani ya kikosi cha Yanga SC ni lazima afanye kazi kubwa kumshawishi mwalimu Miguel Gamondi.

Molinga ambaye amewahi kuichezea Yanga amesema kuwa Yanga kwa sasa ina kikosi kipana na wachezaji bora zaidi kuliko nayakati za nyuma.

“Yanga ya sasa hivi lazima utumie akili, Yanga hii wapo Aziz Ki, Chama, Pacome, Maxi wote wana uwezo. Khalid Aucho ana mipira mirefu ambayo inaweza kumfanya mchezaji kufunga.

“Kuna sehemu umefanya vizuri unabaki kwenye historia na kupita tu unakuwa umeacha historia, sio kukaa kuifikiria Yanga eti nirudi, kila mtu anamuda wake wa kukaa na kuondoka Yanga, waliopo kwa sasa ndio muda wao wa kupata hela na kujulikana,” amesema David Molinga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: