Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Molinga, Sibomana wazua jambo Yanga

73525 Molinga+pic

Fri, 30 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera akitaja uchovu kama sababu ya timu yake kupoteza mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting juzi, ubutu wa washambuliaji wake unaweza kuwa chanzo cha matokeo hayo.

Zahera alisema uchovu wa wachezaji wake kutokana na kutopata muda wa kutosha wa kupumzika uliwagharimu kwa namna moja au nyingine katika mechi dhidi ya Ruvu Shooting waliofungwa bao 1-0 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Hakuna namna ambayo washambuliaji wa Yanga wanaweza kukwepa lawama kutokana na ufanisi mdogo walionao katika kufunga jambo linaloiweka timu hiyo hatarini msimu huu.

Washambuliaji waliocheza jana ni Juma Balinya, David Molinga, Patrick Sibomana na Sadney Khoetage ambao ni raia wa kigeni.

Wachezaji wa Yanga wanaocheza nafasi ya ushambuliaji, wameonekana kukumbwa na tatizo la kukosa umakini na utulivu wa kutumia nafasi wanazopata katika lango la timu pinzani licha ya kutengeneza nafasi za kutosha za mabao.

Hali hiyo imechangia Yanga kujikuta ikifunga mabao machache ambayo yanatokana na mipira iliyokufa kama penalti, kona na faulo badala ya yale yanayotokana na nafasi ambazo zinatengenezwa.

Pia Soma

Advertisement   ?
Katika mechi nne za mwisho ilizocheza Yanga imefunga mabao matatu tu ambayo hakuna lililotokana na nafasi ilizotengeneza na badala yake ilikuwa ni mipira ya kutenga ma kona.

Bao la kwanza kati ya matatu hayo ni lile ambalo Yanga ilifunga katika sare ya bao 1-1 dhidi ya Township Rollers kwenye mechi ya kwanza nyumbani na hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambalo lilitokana na mkwaju wa penati iliyopigwa na Papy Sibomana.

Bao la pili dhidi ya AFC Leopards ambayo Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na kiungo Tshishimbi aliyeunganisha kwa kichwa mpira wa kona ambayo Yanga ilishinda dakika za jioni.

Jingine la tatu ni lile lililowapa ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Township Rollers ambalo lilifungwa kwa njia ya mkwaju wa faulo iliyochongwa na Juma Balinya baada ya wapinzani wao kufanya faulo nje kidogo ya eneo la hatari.

Katika kudhihirisha ubutu wa safu ya ushambuliaji ya Yanga, kwenye mechi ya juzi dhidi ya Ruvu Shooting, licha ya timu hiyo kupiga mashuti 9 yaliyolenga lango, haikufunga hata bao la kuotea wakati wapinzani wao walipiga mashuti mawili tu na kati ya hayo, moja lilizaa bao.

Chanzo: mwananchi.co.tz