Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mokwena uso kwa uso na Guardiola, Ancelotti

Rhulani Mokwena Sdfe Mokwena uso kwa uso na Guardiola, Ancelotti

Wed, 22 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Mamelodi Sundowns FC, Rhulani Mokwena amepata mualiko kutoka Shirikisho la Mpira Ulimwenguni (FIFA) Kwenye upangaji wa Makundi ya Michuano ya Vilabu Ulimwenguni yaani FIFA Club World Cup utakaofanyika Mwezi ujao huko Marekani.

Atajumuika pamoja na moja ya Makocha kutoka Bara la Ulaya ambao Klabu zao pia zimeteuliwa Kushiriki michuano hiyo.

Makocha hao ni Pep Guardiola wa Manchester City, Pamoja na Carlo Ancelotti wa Real Madrid.

Mbali na Rhulani Mokwena pia Kocha wa Al Ahly ya Misri, Marcel Koller amepokea mualiko huo.

Ikumbukwe pia Mamelodi ni Moja ya Klabu kutoka Afrika ambayo imepata tiketi ya Kufuzu Michuano hiyo iliyopewa thamani kubwa sana Kwa sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live