Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mokwena kuwa kocha msaidizi wa Nabi?

Mokwena Nabi Fdg Mokwena kuwa kocha msaidizi wa Nabi?

Wed, 3 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashabiki wa soka nchini Afrika Kusini wameonesha kuguswa na ripoti kwamba Kocha Mkuu wa Mamelodi Sundowns, Rhulani Mokwena mwenye umri wa miaka 37 huenda akawaacha mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Soka nchini humo.

Mamelodi Sundowns watakuwa chini ya kocha mpya wa kuwaongoza msimu ujao baada ya ripoti kuibuka kuwa huenda Rhulani Mokwena akaondoka.

Kocha huyo ameiongoza klabu hiyo tangu mwanzoni mwa msimu wa 2022/23 alipopewa jukumu pekee la kuongoza timu ya ufundi mbele ya Manqoba Mngqithi na Steve Komphela.

Wakati baadhi ya mashabiki wa Mzansi wakiamini kuondoka kwake kutaisaidia timu hiyo kujenga benchi jipya la ufundi ambalo wanaamini litawapa mafanikio kwani wanao wachezaji bora.

Wengine wanaamini itakuwa fursa kubwa kwake kuthibitisha ubora na thamani yake katika timu nyingine na ligi.

Inaelezwa kuwa, Mokwena anaweza kujiunga na Kaizer Chiefs kama kocha msaidizi kwani tayari wameshasajiri kocha mkuu ambaye ni Nassredine Nabi lakini inatajwa kwamba Mokwena ana upendeleo kwenye kupanga kikosi, jambo ambalo hata Kaizer wenyewe wanalitafakari kabla ya kuamua kumchukua.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live