Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mokwena anamtaka Percy Tau pale Wydad

Percy Tau Egypt Mokwena anamtaka Percy Tau pale Wydad

Thu, 22 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Klabu ya Wydad Athletic, Hicham Ait Menna amesema ni kweli waliulizia huduma ya Winger, Percy Tau (30) .

Percy Tau amekuwa hapati nafasi katika kikosi cha Al-Ahly mwishoni mwa msimu wa 23|24. Kutokana na ukaribu wa Percy Tau na aliyewahi kuwa kocha wake Mamelodi Sundowns, Rhulani Mokwena Wydad wanajaribu bahati yao kumshawishi.

Al-Ahly Cairo wamepanga kumuuza au kumtoa kwa mkopo, Percy Tau iwapo tu wakipata mbadala wake kwa sababu kanuni za Egypt zinaruhusu kusajili idadi ya wachezaji (5) pekee wa kigeni.

Tayari Mokwena ameshampata mchezaji wake wa zamani pale Mamelodi, Cassius Mailula ambaye amejiunga na Wydad Athletic kwa mkopo, ametangazwa leo jioni akitokea Toronto FC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live