Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mokwena amwaga machozi, Mamelodi ikitwaa ubingwa AFL

Mokwena Sundownss Mokwena amwaga machozi, Mamelodi ikitwaa ubingwa AFL

Mon, 13 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Mamelodi Sundowns, Rhulani Mokwena alijikuta akishindwa kujizuia na kumwaga machozi uwanjani baada ya filimbi ya mwisho ya mchezo wa fainali yapili ya African Football League (AFL) dhidi ya Wydad Casablanca.

Mokwena alionekana akirukiwa na kuzongwa na wachezaji wake sambamba na benchi la ufundi wakati akitembea kuingia uwanjani huku akimwaga machozi ambayo yanatafsiriwa kuwa ni furaha iliyozidi baada ya timu yake kuchukua ubingwa.

Mashindano hayo ambayo yametamatika leo Novemba 12, yameshuhudiwa yakiweka historia ya kumpata bingwa wa kwanza ambaye ni  Mamelodi baada ya kuifunga Wydad Casablanca mabao 2-0 na kufikisha idadi ya mabao 3-2 katika  matokeo ya jumla kwa mechi zote ya mkondo wakwanza na wapili.

Mchezo wa fainali ya kwanza uliopigwa pale Morocco, ulimalizika kwa Wydad kushinda mabao 2-1, hivyo ilihitaji sare ya aina yoyote ili kuchukua taji hilo lakini ilishindikana.

Mamelodi ilijipatia bao la kwanza katika mechi hii kupitia Peter Shalulile dakika ya tatu ya nyongeza ya kipindi cha kwanza.

Jahazi la Wydad likazamishwa kabisa katika kipindi chapili dakika ya 53 baada ya Aubrey Modiba kufunga bao la pili ba kufanya matokeo ya jumla kuwa 3-2.

Michuano hiyo ambayo imefanyika kwa mara ya kwanza barani hapa, ufunguzi wake ulifanyika Tanzania katika dimba la Mkapa Oktoba 20 ambapo Simba ilicheza dhidi ya Al Ahly na ikatoka sare ya mabao 2-2.

Jumla ya timu nane zilishiriki michuano hii huku Afrika ya Kaskazini ikionekana kutawala zaidi kwa kuingiza timu tatu ambazo ni Al Ahly, Wydad Casablanca na Esperance huku nyingine zilikiwa ni Simba, Mamelodi Sundowns, Simba, Enyimba na TP Mazembe

Chanzo: www.tanzaniaweb.live