Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mokwena alivyotua Chamazini

Mokwena 394396 Kocha Rhulani Mokwena akikabidhiwa jezi ya Azam FC

Fri, 29 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Mamelodi Sundowns, Rhulani Mokwena anatoka katika familia ya soka kweli kweli. Baba yake mzazi ni Julias Sono, gwiji was klabu ya Orlando Pirates.

Julias Sono ni mdogo wa baba mzazi wa Jomo Sono, gwiji mwingine wa soka la Afrika Kusini.

Kwa hiyo Rhulani Mokwena na Jomo Sono ni mtu na mdogo wake, mtoto wa baba mdogo na baba mkubwa. Jomo Sono ndiyo mwanzilishi na mmiliki wa timu ya Jomo Cosmos ya Afrika Kusini.

Akiwa na miaka 37 tu, Rhulani Mokwena anatajwa kama mmoja wa makocha wenye uwezo mkubwa sana kimbinu baranı Afrika…akifananishwa na Pep Guardiola.

Mwaka 2017, akiwa sehemu ya benchi la ufundi la Mamelodi Sundowns, Rhulani alikuja Tanzania kucheza mechi ya kirafiki na Azam FC.

Mchezo huo uliofanyika uwanja wa Mkapa na kuisha kwa sare ya 0-0, ulimfanya Rhulani kugandwa kichwani na jina la Azam FC.

Wakati huo Mamelodi walikuwa mabingwa wa Afrika na walikuwa wakichinja kila aliyepita mbele yao.

Kwa hiyo sare dhidi ya Azam FC ilimshangaza, siyo tu Rhulani, lakini hata kocha mkuu wa wakati ule, Pitso Mosimane…alichokisema Pitso Mosimane kipo kwenye posti ijayo.

Mwaka jana, Mamelodi Sundowns walikuja Tanzania kucheza na Bunamuru ya Burundi, kwenye dimba la Azam Complex.

Akiwa hapa, Rhulani akafurahi sana kukutana tena na Azam FC na kufika makao makau ya klabu.

Akasema anatamani siku moja aje na Mamelodi kucheza na Azam FC akiwa kama kocha mkuu, tofauti na wakati ule alipokuwa msaidizi.

Akasema anaiona Azam FC kama Mamelodi kwani inatumia Irizar kama wao na hata asılı yao ni Brazil kama wao.

Akasema “sisi wenye asılı ya Brazil hatupaswi kutengana”, mwisho wa kunukuu.

Akachukua jezi nyeupe na kuondoka nayo.

Huyo ndiyo Rhulani Mokwena, kocha bora kijana baranı Afrika!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live