Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mokwena: Nipo tayari kufukuzwa Mamelodi

Rulani Mokwena Mchezo.jpeg Kocha Mokwena

Sat, 27 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Mamelodi Sundowns, Rulani Mokwena amejitetea baada ya kipigo cha pili kutoka kwa ES Tunis na kuondoshwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika hatua ya nusu fainali.

Mokwena amesema kuwa yupo tayari kuwajibishwa endapo uongozi wa timu hiyo utaona inafaa huku akidai kuwa yeye bado anaipenda Mamelodi na anatamani kuendelea kusalia katika klabu hiyo lakini endapo wataamua kumtimu atapokea maamuzi ya uongozi.

Mamodi imecheza michezo minne ya CAFCL bila kufunga hata bao moja (robo fainali mbili dhidi ya Yanga walitoa sare ya bila kufungana, nusu fainali mbili amefungwa bao moja kila mchezo na Esperance de Tunis).

"Naitaji Kubaki naipenda Timu hii lakini pia kama awaniitaji nitaondoka na kuwachia timu hii.

“Skuwahi kukimbia Timu hii. Niko hapa kwa sababu ya matokeo mazuri tuliyowahi kuyapata kabla ya leo na kama ayakuwa matokeo mazuri basi nisingelikuwa Hapa.

"Naitaji Kuwa hapa naipenda Timu hii, Nawapenda Mashabiki lakini pia napendezwa na kundi zuri la Wachezaji hawa. Na haya yaliyotokea ni matokeo yaliyopangwa kuwa hivi atukupangiwa kigne,” amesema Rulani Mokwena.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live