Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mokwena: Mechi ya Yanga tunahitaji mashabiki kuliko mechi yoyote

Rulani Mokwena Mchezo.jpeg Rhulani Mokwena

Thu, 4 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Mchezo wa juzi wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini kati ya Mamelodi Sundowns dhidi ya Richards Bay kwenye ligi kuu ya Afrika Kusini, Kocha Mkuu wa Mamelodi Rulani Mokwena alifanya Interview baada ya Mchezo.

Kwenye interview hiyo Mokwena alisema Mchezo wa Ijumaa dhidi ya YANGA ni mchezo pekee ambao wanahitaji Mashabiki wao kuliko mchezo wowote ule kwenye Msimu huu wa 23/24 .

Huyo ni Rhulani ambae anakaa kwenye Benchi la Ufundi na aliishuhudia Yanga pale BENJAMIN MKAPA na kuisoma kiufundi lakini anaonesha hofu dhidi ya YANGA.

Kwenye Msimu wa 22/23 klabu ya Yanga haikupoteza Mchezo wowote ule wa Ugenini kwenye CONFEDERATION CUP kuanzia hatua ya Robo fainali hadi Fainali lakini pia hatua ya Kufuzu kuingia Group Stage ilishinda Ugenini.

Unaweza kuja na Fact yakwamba CONFEDERATION ni kombe la Walioferi lakini hadi sasa hivi ASEC ana uwezekano wa kwenda Nusu fainali yapili kwenye Michuano ya AFRICA ,22/23 Confederation na Sasa anaisaka nusu fainali nyingine ya Champions League.

Yanga alimfunga Usm Alger ya Benchika palepale kwao Omar Stadium ,Tena anampigia mpira ambao unasema hapa angekuwepo Aucho au Feisal hawa Waarabu wangetapika hili kombe.

Kwa Matukio hayo unaelewa ni kwanini Rhulani Mokwena anaongea mambo hayo ya kuhitaji Full House kwao , Yanga ikiwa Ugenini inaogopwa sana tukiacha ile Nabii hakubaliki kwao.

Yanga ikiwa Away ni Hadithi ya Anaconda kwenye Msitu wa Amazon ,Yanga akiwa nje ni sawa na Vampire ameona Damu kwenye shingo la Binadamu ni lazima watu waihofie lakini Tanzania tunaichukulia Yanga kiurahisi sana .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live