Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mokwena: Kabla hujasajiliwa Mamelodi, lazima tujue tabia yako

Rhulani Mokwena.png Rhulani Mokwena.

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kochqa Mkuu wa Klabu ya Mamelodi Sundowns ya nchini Afrika Kusini, Rhulani Mokwena amesema kuwa, timu hiyo haisajili mcheza kabla ya kumchunguza tabia zake ndani na nje ya uwanja.

Mokwena anayekinoa kikosi hicho cha Mabingwa wa African Football League amesema kuwa, sifa kubwa ya mchezaji kusajiliwa ndani ya Masandawana ni lazima awe na tabia njema kabla ya kuwa na kiwango kizuri ndani ya pitch.

"Mamelodi Sundowns hatusajili mchezaji kama hatujui tabia yake ndani ya Uwanja nje ya Uwanja, kitu kikubwa tunafatilia historia yake yote ya hapo awali.

"Watu wanaomzunguka marafiki zake yaani watu walio karibu na mchezaji, hivyo kama akizungukwa na watu wenye Tabia mbaya hawezi kuja Mamelodi Sundowns.

"Unapoichezea sundowns ni lazima uwe binadamu mzuri, hilo ndilo jambo la kwanza. Je, wewe ni mtu mzuri?

"Mamelodi Sundowns hatutaki mchezaji ambaye atataka kuwa mkubwa zaidi ya wenzake ndiyo maana lazma tuchunguze kwanza Tabia Yako kabla hatujanasa saini yako .

"Sundows ni familia moja hivyo mtu wa kucheza hapa ni mwenye nidhamu tuu ....huna nidhamu siyo sehemu salama kwako," amesema Kocha Mokwena.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live