Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mokoena kama Kibu tu! aigomea Mamelodi, Ahly watuma ofa

Mokoenaaaa Kiungo wa Mamelodi Sundowns na Timu ya Afrika Kusini, Teboho Mokoena

Sun, 12 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Mamelodi Sundowns na Timu ya Afrika Kusini, Teboho Mokoena amegoma kuongeza mkataba na klabu yake na taarifa zikisema kuwa nyota huyo anataka kwenda kukipiga Ulaya.

Baada ya kiwango kizuri alichoonyesha kwenye michuano ya Afcon na timu yake ya Taifa Bafanabafana, vilabu mbalimbali kutoka ufaransa na uingereza vimevutiwa na mchezaji huyo na kutaka kumsajili ikiwemo Bournemouth.

Pia Mabingwa wa kihistoria wa Afrika kutoka Misri Al AHLY wametuma ofa kwa nyota huyo kujiunga na miamba hiyo ya soka Afrika huku taarifa za ndani zikieleza kuwa ni ngumu kwa Mamelodi Sundowns kumuachia nyota huyo kujiunga na Al AHLY.

Al Ahly wanataka nyota huyo akacheze pamoja Percy Tau ambaye juzi alishinda tuzo ya mchezaji bora kwa wanaume ukanda wa COSAFA.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live