Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mohammed Ouattara aondoka kambini SImba SC

Outtara Mohammed Outtara

Sat, 15 Apr 2023 Chanzo: Dar24

Imebainika kuwa Beki wa kati wa Simba raia wa Ivory Coast, Mohammed Ouattara hatakuwa sehemu ya wachezaji watakaocheza mchezo wa Kariakoo Dabi kesho Jumapili (April 16) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Katika dabi hiyo, Simba SC ndio wenyeji ambao watawakaribisha Young AFricans katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa kuanzia saa 11 jioni kwa saa za Tanzania.

Ouattara ni kati ya wachezaji waliosajiliwa na Simba SC katika usajili wa msimu huu kwa ajili ya kuwapa changamoto ya namba mabeki Joash Onyango na Hennock Inonga.

Taarifa zinaeleza kuwa Ouattara hayupo kambini tangu juzi amerejea nyumbani kwao Ivory Coast kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Mtoa taarifa hizio ameongeza kuwa beki huyo hatakuwepo katika sehemu ya wachezaji watakaocheza dabi hiyo inayotarajiwa kujaa upinzani mkubwa.

“Hii huenda ikawa taarifa mbaya kwa mashabiki wa Simba juu ya beki wao Ouattara kuondoka nchini na kurejea kwao Abdijan, Ivory Coast.

“Beki huyo amerejea nyumbani kwao kwa ajili ya kwenda kuuguza majeraha aliyoyapata tena hivi karibuni akiwa katika mazoezi ya timu hiyo.”

“Quattara anakosekana katika mchezo wa dabi kutokana na majeraha hayo, kwani hayupo kambini kwa muda wa zaidi ya tatu,” amesema mtoa taarifa huyo

Akizungumzia hilo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema: “Timu ipo kambini ikiendelea na maandalizi ya mchezo wa dabi, kuhusu Outtara suala lake lipo katika benchi la ufundi, kwangu alijafika.

Chanzo: Dar24