Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mohamed awazawadia wazazi wake goli dhidi ya African Sports

MOHAMED MUSSA Mohamed awazawadia wazazi wake goli dhidi ya African Sports

Fri, 3 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji mpya wa Simba SC, Mohamed Mussa amelitoa zawadi bao lake alilolifunga dhidi ya African Sports kwa wazazi wake ambao walimtabiria kuwa atafunga.

Mohamed amefunga bao hilo dakika ya 69 baada ya kupokea pasi ya Moses Phiri ikiwa ni la kwanza kwake tangu ajiunge na Simba kutoka Malindi SC ya Visiwani Zanzibar katika dirisha dogo la usajili mwezi Desemba, 2022.

Momahed amesema kabla ya mchezo aliongea na wazazi wake na walimtabiria kuwa kama atapangwa atafunga na ndicho kilichotokea.

"Nimefurahi sana kufunga bao langu la kwanza nikiwa na Simba. Na hili nawazawadia wazazi wangu pia nimefurahi kufunga kwenye mechi kubwa ya mtoano, imeniongezea morali ya kuzidi kupambana kuisaidia timu," alisema Mohamed.

Akizungumzia nafasi yake kikosini, Mohamed amesema;

"Naamini nitapata nafasi ya kucheza Mwenyezi Mungu ni mkubwa, ushindani upo lakini nitapambana."

Kwenye mechi hiyo iliyopigwa Marchi 2, 2023 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar, Simba walishinda 4-0 dhidi ya African Sports mchezo wa Shirikisho la Azam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live