Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mohamed Hussein aahidi ushindi leo Botswana

Tshabalala: Tusikate Tamaa, Tutarudi Kwenye Ubora Wetu Mohamed Hussein aahidi ushindi leo Botswana

Sat, 2 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kapteni Msaidizi wa Simba SC, Mohamed Hussein 'Tshabalala' ameahidi kuondoka na alama zote tatu leo katika mchezo wao dhidi ya Jwaneng Galaxy nchini Botswana.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo unaotarajiwa kupigwa leo Desemba 2, 2023 majira ya saa 10 jioni, Tshabalala amesema, wachezaji wote wana morali ya mchezo huo hivyo wanaamini watapata matokeo.

"Uzuri hali ya hewa ni kama ya nyumbani, wachezaji wote morali ipo juu ukizingatia mara ya mwisho tulipokuja kwenye uwanja huu tulipata matokeo, tunaomba mashabiki watuombee inshallah tutashinda," alisema Tshabalala.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live