Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mogella awachenjia mashabiki Yanga

Mogela Pic Data Mogella awachenjia mashabiki Yanga

Sun, 28 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

STAA wa zamani wa Yanga, Zamoyoni Mogella ameshangaa mashabiki wanaodai Taifa Stars ilifungwa bao 1-0 juzi usiku dhidi ya Guinea ya Ikweta kutokana na kuwa na wachezaji wengi wa Simba inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

Alisema Kocha Kim Poulsen ambaye ni raia wa Denmark amewaona wachezaji hao ndio wanaofaa katika mchezo huo dhidi ya Guinea ya Ikweta licha ya kukosa matokeo, kitu ambacho Watanzania wanatakiwa kuacha kulaumu na kujikita kutafuta suluhisho.

“Mfano kilichotuua sisi ni mfumo uliotumika timu haikuwa na uhai mbele hata kidogo, sasa wanavyosema wachezaji wengi wa Simba ndio mwalimu kaona aliowapanga wanafaa hivyo kupoteza ni matokeo ambayo mbinu zake hazijafanikiwa,”alisema Mogella ambaye ni miongoni mwa wachezaji wa zamani wasioogopa kukosa pale wanapoona mambo hayaendi.

“Tanzania ina vipaji vingi sana, mimi nawasihi TFF (Shirikisho la Soka la Tanzania) wajitahidi kuzalisha vipaji ambayo vitakuwa na manufaa ndani ya timu ya Taifa, bila ya kufanya hivyo ni kazi bure kwa kuwa hata Kocha Kim atalaumiwa bure bila sababu,” alisisitiza.

Kikosi cha Stars kilichoanza juzi usiku kilikuwa hivi; Manula, Kapombe, Tshabalala,Kenedy Juma, Nyoni, Mkude, Msuva, Mzamiru, Feisal, Samatta na Nado.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz