Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Modrick asusia maswali ya waandishi

Lukaaaaaaaaaaaaaaaaa Modrick asusia maswali ya waandishi

Fri, 21 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Nahodha wa timu ya taifa ya Croatia, Luka Modrid alionyesha kuchukizwa na maswali ya mwandishi juu ya umri wa wachezaji wa taifa hilo mara baada ya mchezo dhidi ya Albania na kuamua kuondoka.

Mchezo huo uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2 uliifanya Serbia kusalia na pointi moja baada ya mchezo wa kwanza na swali hilo lilionyesha kumkera nyota huyo wa Real Madrid na kuamua kuondoka wakati akiendelea kuhojiwa.

Mwandishi alimuuliza Modric kama timu yake itachagua nyota wenye umri mkubwa au mdogo dhidi ya Italia na badala ya kujibu Luka alikunja uso na kuondoka.

Modric, 38, ambaye amekuwa tegemeo katika kikosi cha Croatia tangu aanze kukichezea hadi sasa, mechi dhidi ya Italia inaweza kuwa ndio ya mwisho kwake kwani baada ya michuano hii anaweza kustaafu kutokana na umri.

Hadi kufikia fainali zijazo za Kombe la Dunia, Modric atakuwa amefikisha umri wa miaka 40 na inaelezwa itakuwa ngumu kwake kuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa na ni wazi hii ndio michuano yake ya mwisho kwa ngazi ya timu za taifa.

Katika maisha yake na kikosi cha Croatia, mwaka 2018 ndiyo utakumbukwa zaidi baada ya aliifikisha fainali ya Kombe la Dunia na kupoteza mbele ya Ufaransa. Hadi sasa amecheza mechi 177 na kufunga mabao matano.

Mbali ya timu ya taifa, Modric pia haonekani kuwa na maisha marefu kwenye soka la klabu na akiwa na Madrid ameshinda mataji sita ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na manne ya La Liga.

Chanzo: Mwanaspoti