Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Modric anavyojiandaa kustaafu kishua

Luka Mo Modric anavyojiandaa kustaafu kishua

Sun, 21 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Julai 17, mwaka huu kiungo wa Real Madrid, Luka Modric alisaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia timu hiyo kwa miaka msimu ujao.

Luka ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 38, ifikapo Septemba mwaka huu atakuwa anatimiza 39 na hadi anamaliza mkataba wake kwa msimu ujao atakuwa amebakisha miezi kadhaa kabla yakuwa na miaka 40.

Taarifa zinaeleza huenda huu ndio ukawa msimu wake wa mwisho kuichezea Madrid na kucheza soka kwa ujumla kutokana na umri wake, lakini atakuwa anaondoka katika soka akiwa na utajiri wa kutosha utakaomfanya kuishi kishua bila ya shida yoyote. Hapa tumekuletea mali anazomiliki na jinsi anavyopiga pesa.

ANAPIGAJE PESA

Kiujumla anakadiriwa kuwa na utajiri unaokadiriwa kufikia Dola 75 milioni na kwa mwaka katika mkataba wake mpya anakunja Euro 10 milioni ambayo kwa wiki hupata Euro 200,000.

Kabla ya hapo alikuwa mmoja kati ya wachezaji wanaolipwa zaidi Madrid alipokuwa akipata karibia Euro 500,000 kwa wiki.

Katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi staa huyu anaripotiwa kuwa alipata zaidi ya Pauni 4 milioni kama pesa ya usajili kwa kuongeza mkataba na mwaka huu amepata karibia Euro 2 milioni.

Jamaa anapata mpunga wa kutosha pia kupitia madili mengine ya nje ya uwanja ambapo ana mkataba wa ubalozi na kampuni ya Nike Sofa Score, Oly Bet, Russell Brown na MAX TV ambazo zote zinamuingizia kiasi kisichopungua Pauni 10 milioni kwa mwaka.

NDINGA

Anapenda sana kuendesha magari ya kifahari lakini ndinga nyingi alizokuwa nazo ni kutoka kampuni ya Audi Q7na anamiliki matoleo yote mapya ya kila mwaka yanayotolewa na kampuni hiyo kuanzia mwaka 2016, 2017, 2019, 2020 na 2021, Vilevile ana Bentley Continental GT, thamani ya ndinga zote alizokuwa nazo inakadiriwa kufika Dola 800,000 ambazo ni zaidi ya bilioni moja za Kitanzania.

MSAADA KWA JAMII

Kila mwaka anaripotiwa kutoa zaidi ya Pauni 500,000 kwa mwaka kwa ajili ya kusaidia taasisi za Arthur Rank Hospice Charity sambamba na kampeni ya kupambana na kansa iitwayo Beat Up Cancer.

MJENGO

Alinunua nyumba ya kirahari huko jijini Madrid mwaka 2019 kwa Euro 12 milioni, mjengo huo una ukubwa wa kilomita za mraba 2,700 na ipo katika eneo lenye ukubwa wa kilomita za mrada 10,000.

Ina nyumba tisa, ukumbi wa sinema wenye viti 18, pia kuna baa kwa ajili ya kujivinjari.

Kuna chumba maalumu kwa ajili ya watoto wake kucheza, bwawa la kuogelea na viwanja vya michezo mbali mbali.

MAISHA BINAFSI

Luka sio mtu wa starehe sana, inaelezwa anapenda sana kukaa na familia yake pale anapokuwa mapumzikoni ndio maana katika nyumba yake ameweka vitu vyote muhimu atakavyohitaji awapo mapumzikoni.

Muda mwingi anapokuwa hayupo kwenye majukumu ya kimpira hupendelea sana kulala na kucheza soka kwenye viwanja vilivyo ndani ya nyumba yake.

Kwa sasa yupo kwenye ndoa na mrembo Vanja Bosnic ambaye amezaa naye watoto watatu.

Chanzo: Mwanaspoti