Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Modric amcheleweshea Mbappe jezi namba 10

Luka Modric With Carlo Ancelotti Modric amcheleweshea Mbappe jezi namba 10

Wed, 5 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kylian Mbappe atakosa nafasi ya kupata namba ya ndoto zake atakapotua Real Madrid baada ya Luka Modric kukubali kusaini dili jipya.

Mbappe alikamilisha ndoto zake za kujiunga na Real Madrid kwa uhamisho wa bure na kusaini mkataba wa miaka mitano utakaomsuhudia akilipwa Pauni 12.8 milioni kwa mwaka.

Alitarajia kupewa jezi yenye Namba 10 mgongoni, ambayo ilivaliwa na magwiji kama Luis Figo, Clarence Seedorf, Mesut Ozil na Ferenc Puskas, lakini sasa itamlazimu kusubiri walau kwa mwaka mmoja zaidi ili kupata fursa ya kuvaa jezi hiyo.

Modric kwa sasa ndiye anayevaa jezi Namba 10 na kinachoelezwa ni kwamba amesaini mwaka mmoja ambao ataendelea kubaki Bernabeu.

Na kwa mujibu wa Le Parisien, Modric, ambaye ni mshindi wa Ballon d’Or mwaka 2018, ataendelea kuvaa jezi Namba 10 licha ya usajili wa Mbappe.

Ripoti hizo zinadai kwamba Mbappe sasa atavaa jezi yenye Namba 9, ambayo ipo wazi tangu Karim Benzema alipoondoka kwenda kukipiga kwenye kikosi cha Al-Ittihad inayoshiriki mikikimikiki ya Saudi Pro League.

Supastaa Cristiano Ronaldo alivaa jezi Namba 9 kwenye msimu wake wa kwanza Real Madrid kabla ya kupewa Namba 7 baada ya gwiji wa klabu, Raul kuondoka na kutimkia zake FC Schalke 04.

Na sasa Mbappe anaweza kupita kwenye njia hizo za Ronaldo kwa kuvaa jezi yenye namba nyingine kabla ya kupata fursa ya kuchukua Namba 10, wakati Modric atakapoondoka kwenye kikosi hicho.

Modric alisema atapenda kustaafu soka akiwa kwenye kikosi cha Real Madrid, ambapo kwa msimu ujao, mchezaji huyo atatimiza umri wa miaka 39.

“Daima nimekuwa nikisema nitapenda kustaafu soka nikiwa hapa Real Madrid,” alisema Modric.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live