Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moallin afichua siri kiwango KMC

Moallin Azam DC Kocha Mkuu wa KMC, Abdihamid Moallin

Thu, 12 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu wa KMC, Abdihamid Moallin amesema sababu kubwa ya timu hiyo kufanya vizuri ni ushirikiano uliopo baina yake na wachezaji.

Akizungumza na Mwanaspoti, Moallin aliyeshinda tuzo ya kocha bora kwa mwezi Septemba alisema anafurahia kufanya kazi na kundi kubwa la vijana wenye vipaji huku akiahidi mambo makubwa zaidi.

“Tumeanza vizuri, lakini ligi bado ni ndefu na tunahitaji kufanya zaidi ya tulivyoanza. Nahitaji mwendelezo huo kuona ukiendelea na ndilo jambo ambalo nimekuwa nikiongea na wachezaji ili wasijisahau sana,” alisema.

Moallin aliongeza kuwa licha ya ligi kusimama, lakini wachezaji wake hawatapumzika muda mrefu kwani lengo lake ni kuona hawapotezi muunganiko katika kipindi chote ambacho kikosi hicho hakitacheza.

“Baada ya mchezo na Ihefu tulitoa mapumziko ya siku tatu kwa wachezaji kujumuika na familia zao na leo (juzi) wataanza rasmi kuingia kambini kwa ajili ya kuendelea na mazoezi huku tukitafuta michezo mingi ya kirafiki,” alisema.

Ushindi ilioupata KMC wa bao 1-0 dhidi ya Ihefu ulikuwa wa tatu mfululizo baada ya kuifunga JKT Tanzania na Geita Gold kwa mabao 2-1 kila moja na kuifanya ifikishe pointi 10 hivyo kujisogeza kutoka nafasi ya tano hadi ya nne amesema sababu kubwa ya timu hiyo kufanya vizuri ni ushirikiano uliopo baina yake na wachezaji.

Akizungumza na Mwanaspoti, Moallin aliyeshinda tuzo ya kocha bora kwa mwezi Septemba alisema anafurahia kufanya kazi na kundi kubwa la vijana wenye vipaji huku akiahidi mambo makubwa zaidi.

“Tumeanza vizuri, lakini ligi bado ni ndefu na tunahitaji kufanya zaidi ya tulivyoanza. Nahitaji mwendelezo huo kuona ukiendelea na ndilo jambo ambalo nimekuwa nikiongea na wachezaji ili wasijisahau sana,” alisema.

Moallin aliongeza kuwa licha ya ligi kusimama, lakini wachezaji wake hawatapumzika muda mrefu kwani lengo lake ni kuona hawapotezi muunganiko katika kipindi chote ambacho kikosi hicho hakitacheza.

“Baada ya mchezo na Ihefu tulitoa mapumziko ya siku tatu kwa wachezaji kujumuika na familia zao na leo (juzi) wataanza rasmi kuingia kambini kwa ajili ya kuendelea na mazoezi huku tukitafuta michezo mingi ya kirafiki,” alisema.

Ushindi ilioupata KMC wa bao 1-0 dhidi ya Ihefu ulikuwa wa tatu mfululizo baada ya kuifunga JKT Tanzania na Geita Gold kwa mabao 2-1 kila moja na kuifanya ifikishe pointi 10 hivyo kujisogeza kutoka nafasi ya tano hadi ya nne

Chanzo: Mwanaspoti