Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mo Salah kubaki Liverpool kwa masharti

Mo Salah S Winga wa Liverpool, Mohammed Salah

Wed, 20 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Winga wa Liverpool, Mohamed Salah ameripotiwa yupo tayari kubaki Anfield zaidi ya msimu ujao lakini kama tu mambo mawili yatafanyika.

Kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi, staa huyo alihusishwa sana na mpango wa kutimkia huko Saudi Arabia, wakati Al-Ittihad ilipoweka mezani Pauni 150 milioni kunasa saini yake, lakini Liverpool iligoma kumuuza ikitaka afanye jambo chini ya Kocha Jurgen Klopp.

Alhamisi iliyopita, Salah alifunga bao la tatu la Liverpool kwenye ushindi wa 6-1 kwenye Europa League dhidi ya Sparta Prague na kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao 20 kwa misimu saba mfululizo.

Mabao 206 katika mechi 336 alizochezea Liverpool pamoja na kuasisti mara 92, Mo Salah anazidiwa na wachezaji wanne tu, Ian Rush, Billy Liddell, Gordon Hodgson na Roger Hunt kwenye ishu ya kufunga.

Kinachoelezwa, Mo Salah atakuwa na furaha kubaki kwenye kikosi cha Liverpool kama atahakikishiwa na mabosi wa timu hiyo mambo yataendelea kuwa mazuri.

Mo Salah anataka kufahamu hatima ya timu hiyo mipango yao ipoje huku akitaka kutambua chaguo la kocha atakayekuja kuchukua mikoba ya Klopp, ambaye atakusanya virago vyake na kuondoka mwishoni mwa msimu.

Kuna makocha wengi wanahusishwa na Liverpool akiwamo Xabi Alonso wa Bayer Leverkusen, lakini kocha huyo amekuwa kwenye rada za miamba mingine pia wakiwamo Bayern Munich, Barcelona na Real Madrid.

Kinachoelezwa, Mo Salah anataka afahamu ni kocha gani atakuja kuchukua mikoba, huku akiona mipango ya baadaye ya timu hiyo kujua kama kuna maisha au achukue virago vyake aondoke mwishoni mwa msimu.

Chanzo: Mwanaspoti