Mshambuliaji wa Timu ya Liverpool, Mohamed Salah amevunja ukimya na kutuma ujumbe mzito akiomba kusitishwa kwa kile alichokiita kuwa ni mauaji ya halaiki Gaza.
Katika video fupi aliyoisambaza kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii, Salah amesema misaada ya kibinadamu inapaswa kuruhusiwa mara moja kuingia katika eneo la Wapalestina lililozingirwa.
Salah ambaye ni raia wa Misri, ametoa maoni hayo kwa mara ya kwanza juu ya mzozo unaondelea kati ya Israel na Palestina, baada ya kukumbana na ukosoaji mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, mashabiki zake wakimshinikiza aseme neno ili kuwasaidia Wapalestina.
“Sio rahisi siku zote kuzungumza wakati kama huu, kumekuwa na vurugu nyingi na ukatili mwingi unaoumiza moyo. Maisha yote ni matakatifu na lazima yalindwe,” Salah alisema.