Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mo Salah atuliza presha Liverpool

Mohammed Salah 2 Goals.jpeg Winga wa Liverpool, Mohammed Salah

Wed, 22 May 2024 Chanzo: Mwananchi

Supastaa, Mohamed Salah ametuliza hali ya hewa huko Anfield baada ya kufichua anafikiria kuendelea kubaki Liverpool hadi msimu ujao.

Gwiji huyo wa Liverpool, Mo Salah amekuwa akihusishwa na mpango wa kuachana na miamba hiyo ya Anfield baada ya Jurgen Klopp kuondoka mwishoni mwa msimu huu.

Mkataba wa Salah huko Liverpool utafika tamati, Juni 2025 na kuna dili la pesa nyingi kutoka Saudi Arabia. Staa huyo alikuwa kwenye mpango wa Al-Ittihad iliyoripotiwa kuweka mezani Pauni 170 milioni.

Klabu hizo za Mashariki ya Kati zinaripotiwa huenda zikarejea tena Anfield dirisha hili la majira ya kiangazi na kinachoelezwa Pauni 200 milioni zitawekwa mezani kunasa saini yake.

Baada ya msimu wa Ligi Kuu England kufika tamati Jumapili iliyopita, Mo Salah aliposti picha kwenye mitandao ya kijamii akiwa uwanjani Anfield pamoja na mabinti zake wawili, Makka, 10, na Kayan, 4.

Kisha alituma ujumbe kwenye Twitter kuhusu Klopp, alipoandika: "Ilikuwa wakati mzuri kushinda mataji yote yale tukiwa pamoja na kupata uzoefu mkubwa kwa zaidi ya miaka saba. Nakutakia kila la heri katika maisha yako mengine, natumaini tutakutana tena."

Kisha Salah aliweka posti nyingine ambayo ilionyesha atabaki Liverpool kwa msimu ujao.

Alisema: "Tunajua mataji ndicho kitu kinachohesabika na tutafanya kila kinachowezekana msimu ujao iwezekane. Mashabiki wetu wanastahili hili na tunapambana kwa nguvu zote."

Arne Slot, amethibishwa kuwa kocha mpya atakayeinoa timu hiyo kuanzia msimu ujao. Kocha huyo Mdachi ameripotiwa kusaini mkataba wa miaka mitatu huko Anfield.

Chanzo: Mwananchi