Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mo Salah afunga"hat trick" Liverpool ikiikukung'uta Man United 5-0

Cf44cc23e16e14f5 Mo Salah afunga"hat trick" Liverpool ikiikukung'uta Man United 5-0

Sun, 24 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Man United wamepokezwa kichapo cha mwaka katika historia ya soka baada ya kupigwa mabao matano kwa bila na mahasidi wao Liverpool ugani Old Trafford.

Mechi hiyo kali ya Ligi Kuu Uingereza ilimshuhudia Mohamed Salah aking'aa huku akifungia Reds mabao manne na kuzamisha chombo cha United.

Mashetani Wekundu waliingia katika mechi hiyo wakijivunia ushindi wa 3-2 dhidi ya Atalanta katika mechi ya Ligi ya Mabingwa mapema wiki hii.

Hata hivyo, masogora wa Ole Gunnar Solskjaer walishindwa kuendeleza ubabe huo na kuongeza masaibu yao katika mechi hiyo ya nyumbani.

Wageni walitawala idara zote za mechi hiyo huku Naby Keita akifungua ukurasa wa mabao katika dakika ya tano ya mchezo baada ya Bruno Fernandes kupoteza nafasi nzuri ya kufunga bao.

Diogo Jota alisawazisha bao hilo dakika nane baadaye akichuma nafuu kutoka kwa masihara ya Luke Shaw na Harry Maguire.

Mason Greenwood alikaribia kufungia United katika dakika ya mwisho kuingia muda wa mapumziko kabla ya Salah kufanya mambo kuwa 3-0 akimalizia vyema krosi.

Mzawa huyo wa Misri alifunga bao lake la pili katika dakika ya kuingia muda wa mapumziko kabla ya kumalizia hat-trick yake punde baada ya kuanza kwa awamu ya pili.

Mambo yalikwenda mrama kwa United kunako dakika ya 60 baada ya Paul Pogba, ambaye aliingia kama mchezaji wa akiba kuliswa kadi nyekundu kwa kucezea rafu Keita.

Mababruvari wa Jurgen Klopp' walisndwa kunufaika na kuounua kwa idaid ya wacezaji wa wenyaji kutwaa mabi zaidi uku wakisikilia usindi wa 5-0.

Ushibdi mkubwa ulitosa Reds kuwpaiku Man City na kuoaa adi nafsi ya pili jedealini uku United wakisuka adi nafsi wya saba.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke