Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mo Salah: Ninamtamani Kevin De Bruyne

Mo Salah X KDB.png Mo Salah: Ninamtamani Kevin De Bruyne

Thu, 30 Nov 2023 Chanzo: Dar24

Mshambuliaji kutoka nchini Misri na Klabu ya Liverpool ya England, Mohamed Salah, amebainisha kwamba, mbali Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, mchezaji ambaye anatamani acheze naye timu moja ni Kevin De Bruyne wa Manchester City.

Wawili hao ilibaki kidogo wacheze pamoja ndani ya Chelsea, lakini haikuwa hivyo baada ya kupishana klabuni hapo na kila mmoja akikaa kwa miaka miwili.

Alianza De Bruyne kuwa mchezaji wa Chelsea, alikaa kuanzia 2012 hadi 2014, kisha Salah akatua hapo mwaka 2014, akaondoka 2016.

“Katika maisha yangu ya soka, ningependa kucheza sambamba na Ronaldo na Messi, lakini mbali na hao, mchezaji ambaye ningetamani kuwa naye timu moja ni Kevin De Bruyne,” amebainisha Salah.

Katika hatua nyingine, Salah amefichua kwamba, ndani ya Premier League, beki mgumu zaidi ambaye amewahi kukutana naye ni Cesar Azpilicueta aliyekuwa akitumikia Chelsea kuanzia 2012 hadi 2023, kabla ya kutimkia Atletico Madrid.

Chanzo: Dar24