Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mo Dewji umemaliza kazi yako, sasa kazi kwa Robertinho

Mo Luis Mo Dewji umemaliza kazi yako, sasa kazi kwa Robertinho

Mon, 24 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni mengi sana yameongelewa kuhusu klabu yetu ya Simba Sc,, kuna mazuri,, kuna mabaya, kuna ushauri,, kuna kukosoa,, nk na hata kutukana pia.

Huyu katika picha ni mtoto kutoka katika familia ya mzee Gulam Dewji muite Mohammed Dewji 'Mo'

Ukiachana na uwekezaji anaoufanya ndani ya klabu yetu ya Simba Sc bado yeye ni shabiki kindaki ndaki wa Simba Sc,, anaweka pesa kwa mapenzi yake yeye,, hajali nini watu wanazungumza juu yake yeye ila anasimamia katika misimamo yake.

Mo Dewji, sisi kama mashabiki lia lia wa klabu hii ya Simba Sc tunasema hatuna tunachokudai mpaka sasa, kazi yako umeifanya ipasavyo, umehakikisha mashabiki wa klabu hii tukirudiki katika furaha ile iliyopotea katika misimu miwili iliyopita.

Wewe pekee ndiye ulitujengea timu mpaka ikawatishio barani Afrika, wewe ndiye uliyefanya timu kama Al ahly, Kaizer Chiefs, Orando Pirates, As Vita Club na zingine nyingi kuogopa kukutana na Simba Sc katika michuano ya CAF pale kwenye Dimba la BWM.

Ulitufanya mashabiki wa timu hii kubwa Tanzania kutembea kifua mbele huku tukitamba kwa ubora tuliokua nao na hayo yote hayakuja tu bali ULIWEKA PESA.

Watu wengi wanatamani kuona ukiondoka katika klabu hii lakini mapenzi yako pekee ndiyo yanakufanya uendelee kuwekeza katika timu hii.

Na sasa tumesha ona umeamua sasa, unataka kuurejesha ufalme wa Simba Sc ndani na nje ya mipaka ya Tanzania,, umeamua kuleta Benchi Bora la Ufundi chini ya Kocha wetu Mbrazili Robertinho pamoja na jopo lake lote la wasaidizi.

Umeamua kuleta wachezaji wa maana wenye hadhi ya ushindani na kuipigania nembo ya klabu hii ya Simba Sc. Japo tunajua sio kila mchezaji anayesajiliwa basi atakuwa bora ila TUNAIMANI wameletwa wachezaji bora zaidi.

Baada ya kilio cha muda mrefu kutoka kwa mashabiki wa klabu hii ya Simba Sc wakitaka kumrudisha kijana wao pendwa zaidi Luis Jose Miquissone umeamua kuwarudishia kijana wao, hii yote tunajua umefanya kwa mapenzi ya dhati kabisa kutoka moyoni.

Na hii ndiyo Simba

Aishi Manula/ Luis Jefferson

Shomari Kapombe/Duchu Kameta

Mohammed Hussein/Israel Mwenda

Malone/Kennedy Juma

Henock Inonga/Hussein

Kazi Sadio Kanoute/Abdullah

Hamis Luis Miquissone/Kibu Denis

Fabrice Ngoma/Mzamiru Yassin

Jean Baleke/Moses Phiri

Clatous Chama/Saido Ntibazonkiza

Aubin Kramo/Willy Onana

Wengine

Ally Salim

Ahmed Feruzi

Nassoro Kapama

Jimson Mwanuke

Shabani Chilunda

John Bocco Mohamed

Mussa na wengine.

Wabaya wasiopenda maendeleo, wasiopenda klabu hii ikisonga mbele wanatamani kuona ukiiacha timu hii, lakini wewe upo bega kwa bega na klabu hii.

Mengi yalisemwa hasa pale waliposikia ile kauli yako kuhusu "KUWEKEZA SIMBA NI HASARA" hawakutambua ugumu unaopitia katika uwekezaji huu,, hawakujua ni mengi mno unapitika katika klabu hii ila kilichokufanya uwe mshindi ni UVUMILIVU wako.

Pale uliposema "Utakata tamaa" wengi walitamani uondoke lakini ukakumbuka unaupendo wa dhati na klabu hii pamoja na mashabiki zake ukaamua kukaa kimya na kuweka pesa zaidi.

Kazi yako umemaliza bosi MO

Mpaka sasa sisi mashabiki wa Simba Sc tunasema hakuna tunachokudai,, tumeshaona pesa umeweka, wachezaji umesajili, kila hitaji la kocha wetu Robertinho umemtimizia .

Kilichobaki sasa ni utekelezaji wa wachezaji wenyewe pamoja na kocha, kuipambania klabu hii iweze kurejesha ufalme wake katika nchi hii na nje ya Tanzania.

Tunashukuru sana sana sana, sasa ni sisi mashabiki jukumu letu lililobaki ni kuwapa sapoti nyie viongozi wetu pamoja na wachezaji kwa ujumla katika kuhakikisha tunapata furaha zaidi.

Mungu aendelee kukupa maisha marefu Mohammed Dewji. Tunampenda sana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: