Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mo Dewji hapa anahusikaje?

Try Again Drg Mo Dewji hapa anahusikaje?

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi anatoa pesa kumsajili kipa kama huyu ambaye uliambiwa kabisa kwa muda ambao alikaa nje na kwa sheria za bodi ya ligi hakutakiwa kusajiliwa ligi yetu, kisa tu ametoka Brazil.

Kiongozi unaingia kwenye account unatoa pesa kumsajili huyu kipa. Ni sawa umemsajili sasa lakini umeambiwa kakaa nje kwa muda mrefu baada umfanyie vipimo unamsajili tu na anaingia mazoezini moja kwa moja.

Hapa anatokea mtu anakwambia Mo hajaweka hisa zake, Mo ni Tapeli, Mo ni Janja Janja, sasa hisa na usajii mbovu wapi na wapi? Hili mnalolipigia kelele hivi sasa mimi niliwahi kuliandika na kama mnakumbuka hadi Mo aliwahi ku-repost ile post yangu iliyokuwa imesomeka kwa title ya "Bila uongozi imara ni bure".

Mo ndiye alimsajili Sawadogo? Wachezaji wanaoletwa sio wa daraja la juu kuifanya Simba ipambane na timu kubwa kama Al Ahly na wengine.

Mo ni kama anaisaidia Simba tu, hakuna muwekezaji seriously atakayekuja Simba na mmwambie mgawane hisa na wanachama na wakati klabu haina hata wanachama hai, yaani mzigo wote mmpe yeye atoe hela halafu hisa za wanachama zisitumike.

Simba tambueni hamuwezi kumpata muwekezaji aina ya Mo ambaye leo hii mnamuita ni tapeli, mwekezaji akija atatakaa hisa zote asilimia 100% na mkikataa atasepa.

Hakuna mfanya biashara atakayeweka hisa na watu ambao hawaweki pesa labda muwekezaji huyo mumwambie hisa hizo agawane na Mo Club ibaki bila wanachama. Vinginevyo mtapata wadhamini tu kama ambao Yanga wamewapata lakini siyo kupata mwekezaji.

Mo huyu huyu ndiyo ameiinua Simba na kuiweka kwenye ramani ya Afrika kuingia robo fainali kwa miaka mitano mfululizo jambao ambalo lilikuwa ndoto huko nyuma, ameipa ubingwa wa Ligi back to back miaka minne mtani wenu akisubiria.

Hata Yanga wenyewe naamini kuna wakati wakiwa wanatembeza bakuli walitamani wapate mtu kama Mo Dewji lakini haikuwezekana.

Tanzania nzima ni Simba tu ndiyo ina muwekezaji, mkitaka Mo atoke hata leo hii atatoka kwani ni mtu ambaye hategemei Simba ili utajiri wake upande ni mtu ambaye ana kampuni na utajiri wa kununua timu zote ambazo zipo ligi kuu pamoja na Championship, Simba mheshimuni Mo, wekeni uongozi mzuri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live