Kabla kikosi cha Simba SC kuingia katika dimba la Mkapa baadae jioni leo Ijumaa (Oktoba 20), Rais wa heshina wa klabu hiyo, Mohanned Dewji ‘Mo’, amekutana na wachezaji wote sambamba na Benchi la Ufundi na kutoa ahadi pamoja na maagizo muhimu.
Simba SC inawakaribisha Al Ahly kwenye Uwanja wa Mkapa, katika mchezo wa African Football League ‘AFL’ ukiwa ni mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo inayoshirikisha klabu nane za Afrika.
Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC , Ahmed Ally amesema, kikosi cha timu hiyo kipo tayari kwa mpambano dhidi ya Al Ahly na Rais wa heshima Mo Dewji amezungumza na wachezaji sambamba na Benchi la Ufundi na kutoa haadi nzito.
“Ni kweli Rais wetu wa heshima Mo Dewji amekutana na Wachezaji sambamba na Benchi la Ufundi, lengo ni kuwapa hamasa ya ushindi ili tuweze kufanya vizuri katika mchezo wetu na Al Ahly na kisha tusonge mbele”
“Kwa upande wa kikosi chetu hadi sasa kipo tayari kwa asilimia 100 kwani kila mchezaji yuko fiti na wanasubiri muda wa kwenda kukupambana ili kuvuna pointi tatu, kwani wachezaji wote kwa maana ya Manula (Aishi) na Inonga (Henock) wapo fiti asilimia 100,” amesema Ahmed Ally