Simba imefichua kuwa mwekezaji wa klabu hiyo, Mohammed Dewji ‘MO’ alichangia Sh2.4 bilioni katika bajeti klabu hiyo kwa msimu wa 2022/2023.
Akitoa taarifa ya fedha ya klabu hiyo ya 2022/2023, Mhasibu wa Simba, Suleiman Kahumbu amesema awali walipanga kukusanya Sh12.3 bilioni kwa msimu huo na mchango wa MO ulichangia kwa kiasi kikubwa wakavula lengo hadi Sh15 bilioni.
“Katika bajeti ya fedha ya msimu wa 2022/23 rais wa heshima wa Simba Mohamed Deji alituchangia kiasi cha Sh2.4 bilioni, fedha ambazo zilienda moja kwa moja kwenye kufanikisha kukusanya bilioni 15 ambazo zimetupa faida kwa kiasi kikubwa,” amesema Kahumbu.
Kahumbu amesema hayo Leo januari 21, 2024 katika mkutano wa mwaka wa klabu hiyo unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam.
“Matumizi ya 2022/23 yalipangwa kuwa Tsh. 12,363,626,983 lakini matumizi halisi ni Tsh. 15,936,829,943. Bajeti kwa mwaka 2023/2024 klabu imepanga kukusanya kiasi cha Tsh. 25,930,722,300 lakini imepanga kutumia kiasi cha Tsh. 25,423,997,354. Tutabaki na mapato ya ziada ya Tsh. 506,724,946.”- Mhasibu wa Klabu, Suleiman Kahumbu