Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mo Dewji alivyoibeba 'Yanga ya Kimataifa'

Mohamed Dewji Mo Dewji Mo Dewji alivyoibeba 'Yanga ya Kimataifa'

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kabla Simba SC haijaenda robo mwaka 2018, miaka miwili nyuma Yanga SC ikiwa chini ya Yusuf Manji ilitinga makundi CAFCC mara mbili ndani ya miaka mitatu kipindi ambacho unaruhusiwa kusajili wachezaji 6 tu wa kimataifa na unaweza kuwatumia wanne tu uwanjani.

Manji akaondoka Yanga mwaka huo huo Mo akaingia Simba, Yanga ikayumba kiuchumi na kuziacha project zake ikiwemo project muhimu iliyopewa jina la "Yanga ya Kimataifa" iliyohusisha pia mabadiliko kutoka Yanga asili kwenda Yanga Company na kuibukia kwenye bakuli.

Simba wakaanza kufanya vizuri ikanogeshwa na kusajili wachezaji 10 wakimataifa na kutumia nane badae wote 10 kutumika. Simba wakaichukua project ya Yanga ya kimataifa na kuihamisha kwao wakisaidiwa na nguvu ya pesa za Mo.

Muda ukapita, Yanga wakiwa wanatafuta wadhamini wakampa timu Dkt. Mshindo Msola (PhD). Akaanzisha safari ya mabadiliko na kwa udhamini wa Azam akaomba kusaidiwa safari hiyo na Sevilla.

Uzuri GSM akaingilia kati safari nzima ya kuibadilisha Yanga na kuipenda proposal ya Msola, hapo ndipo alipoifanya Yanga kama moja ya kampuni zake ili asipate hasara, akamwambia Eng. Hersi Said ahakikishe anapata taarifa zote kuhusu Yanga.

Tukaanza kumuona Hersi akiwa katika shughuli za kiuongozi za Yanga bila kuwa na cheo chochote. Mfano; usajili, uhamasishaji, utiaji saini wa baadhi ya mikataba, uwajibishaji na ulipaji wa huduma za Yanga.

Haikuishia hapo Hersi akawa kama katibu kivuli wa Yanga na baadae kuwa Rais wa Yanga na haya ndio matunda yake. Simba wanasahau mpira wa Tanzania ulikuwepo toka enzi za ukoloni na wala mpira haukuanza 2018. Yalifanyika mengi kabla ya 2018.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: