Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mo Dewji: Wanaobet wanawapa hela wachezaji ili wafungishe Timu

Mo Simba Dewji Rais wa Heshima wa Klabu ya Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’

Wed, 5 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika muendelezo wa Mahojiano ya Rais wa Heshima wa Klabu ya Simba Mohammed Dewji na Global TV sehemu ya tano, Mwekezaji huyo ameibua suala jipya la rushwa klabuni hapo.

Mo Dewji anasema Rushwa ya aina yoyote itaua mpira wa Tanzania au kuua mpira wa Afrika Rushwa itakupa mafanikio kwenye Short term gains laki Long gains hutoweza kufanikiwa.

“Sikubaliani na rushwa ya aina yoyote, lakini nasikia Kuna kampuni zingine au Kuna watu ambao wameingia kwenye betting baadae wana beti alafu wanawatafuta wachezaji wanawaambia fungisheni Timu mpewe hela.

“Hili jambo mimi silipendi, nmeanza kuweka mfumo wa Ki-intelligence ndani ya simba, haiwezekani sisi tunahangaika kuifanikisha Simba isonge mbele alafu kuna mtu/watu ambao kwa namna moja ama nyingine wamehusika kuifungisha Simba kwa ajili ya Rushwa, hawa watu watachukuliwa hatua."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live