Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mo Dewj ateua wajumbe Baraza la Ushauri, Dalali, Rage, Aveva ndani

MO Dewji Apinga Goli Walilofungwa Na Power Dynamos.jpeg Mo Dewj ateua wajumbe Baraza la Ushauri, Dalali, Rage, Aveva ndani

Sun, 29 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

UTEUZI WA WAJUMBE WA BODI YA BARAZA LA USHAURI SIMBA SPORTS CLUB COMPANY LIMITED

Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita tangu tuanze safari ya Mabadililko Klabu yetu imepiga hatua kubwa sana katika nyanja mbali mbali.

Pamoja na maendeleo ambayo Klabu yetu imepiga katika kipindi hiki cha miaka mitano lakini malengo yetu bado hatujayafikia.

Mojawapo ya majukumu yangu kama Rais wa heshima wa Simba ni kuhakikisha Uongozi na Utawala bora unazidi kuboreshwa kila wakati ili kuzidi kusukuma gurudumu la maendeleo ya Klabu yetu.

Hivyo basi baada ya kushauriana na Mwenyekiti wa Bodi na Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, nimewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Baraza la Ushauri (Advisory Board) la Klabu ya Simba.

1. Jaji Thomas Mihayo M/kiti 2. Hassan Dalali-Mjumbe 3. Ismail Aden Rage-Mjumbe 4. Evans Aveva-Mjumbe 5. Faroukh Baghoza 6. Swedi Nkwabi-Mjumbe 7. Azim Dewji-Mjumbe 8. Kassim Dewji-Mjumbe 9. Musleh Al-Ruweh-Mjumbe 10. Mohamed Nassor-Mjumbe 11. Mulamu Ng’ambi-Mjumbe 12. Octavian Mshiu-Mjumbe 13. Prof Janabi-Mjumbe 14. Hassan Kipusi-Mjumbe 15. Geofrey Nyange-Mjumbe 16. Gerald Yambi-Mjumbe 17. Moses Kaluwa-Mjumbe 18.Crescentius Magori-Mjumbe 19. Juma Pinto- Mjumbe 20. Mwina Kaduguda-Mjumbe 21. Idd Kajuna-Mjumbe

Sekretariat ya Simba itaratibu mikutano ya Baraza hili la Ushauri.

Kazi kubwa ya Baraza hili itakuwa ni kuishauri Bodi juu ya maendeleo ya Klabu yetu ya Simba, Uongozi na Utawala bora.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live