Kikosi cha Simba SC kimefanya mazoezi ya mwisho jana katika Uwanja wa nje wa New Amaan Complex kuikabili Jamhuri katika mchezo robo fainali ya michuano ya Kombe Mapinduzi utakaopigwa leo saa 2:15 usiku.
Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na hakuna aliyepata maumivu ambayo yanaweza kumfanya kuukosa mchezo wa kesho.
Uongozi wa Simba umesema kuwa, morali za wachezaji zipo juu na wataingia kwenye mchezo wa leo wakiwa na lengo la kuibuka na ushindi ili tutinge nusu fainali.
Tayari kocha msaidizi wa Simba, Seleman Matola ameweka wazi kuwa haitakuwa mechi rahisi na tunategemea kupata upinzani lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo chanya.